Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Mashirika ya Kimataifa huko Vienna Mikhail Ulyanov aliandika katika chapisho katika kituo chake cha Telegram kwamba nchi yake inajitahidi kuandaa taarifa kama hiyo katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Vienna (UNOV) ya kupinga vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na hatua zozote zilizo dhidi ya Uislamu kama vile kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu.
Alisema kauli hiyo itajadiliwa katika mkutano wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kuzuia Uhalifu na Haki ya Jinai, unaotarajiwa kufanyika Ijumaa hii Desemba 8.
Huko nyuma mwezi wa Juni, Rais wa Russia Vladimir Putin alisema kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu hakuonekani kama uhalifu katika baadhi ya nchi za Magharibi lakini nchini Russia ni kinyume cha sheria na wahusika wanaadhibiwa.
Putin aliongeza kuwa: "Qur'ani ni takatifu kwa Waislamu na inapaswa kuwa takatifu kwa wengine," alisema na kuongeza, "Siku zote tutazingatia sheria hizi."
4186254