IQNA

Ibada

Maelfu ya Waislamu wajiandikisha kwa ajili ya Itikafu kwenye Haram ya Imam Ridha (AS)

18:06 - December 19, 2023
Habari ID: 3478059
IQNA - Zaidi ya Waislamu 70,000 kutoka nchi 22 wamejiandikisha kushiriki katika ibada ya itikafu au itikaf katika Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) huko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran.

Itikafu ni ibada katika Uislamu ambayo inahusisha kukaa msikitini kwa idadi fulani ya siku, ambapo waumini hujishughulisha na ibada mbali mbali zikiwamo kuswali, kusoma Qur'ani Tukufu, dua na saumu.  Itikafu ambayo waumini wamejisajili kushiriki ni ile ya  tarehe 13, 14, na 15 Rajab, mwezi wa saba wa kalenda ya Kiislamu.

Haram ya Imam Ridha (AS), Imam wa nane wa Shia na ambaye ni kutoka kizazi au Ahul Bayt wa Mtume Muhammad (SAW), ni moja ya maeneo matukufu na yanayotembelewa zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu.

Amin Behnam, afisa eneo hilo takatifu, alisema Jumatatu kwamba mchakato wa usajili, ulioanza Desemba 5 na kudumu kwa siku 10, uliwavutia zaidi ya Wairani 67,355 na wageni 3,070.

Amesema raia wa kigeni waliojisajili ni kutoka  nchi 21 zikiwemo Afghanistan, Pakistan, India, Iraq, Uturuki, Lebanon, Australia, Jamhuri ya Azerbaijan, Syria, Nigeria, Marekani, Canada, Bangladesh, Tanzania, Ujerumani, Ufilipino, Kazakhastan, Afrika Kusini, Kuwait, Uholanzi na, na Hinduras.

Aliongeza kuwa 69% ya waliojiandikisha walikuwa wanawake na 31% ni wanaume, na kwamba idara ya eneo hilo takatifu  itatenga maeneo 1,200 ya ibada.

Itikafi hiyo itafanyika kuanzia Februari 24 hadi 26 katika nafasi ya chini ya ardhi ya Msikiti wa Goharshad, msikiti wa kihistoria ulio karibu na eneo hilo takatifu.

Ibada ya itikaf ni mila ya Mtume Muhammad (SAW) na Ahul Bayt wake, na inachukuliwa kuwa ni ibada yenye thawabu nyingi katika Uislamu.

Kishikizo: itikafu imam ridha
captcha