IQNA

Jinai za Israel

Walowezi wa Kizayuni wavamia Msikiti wa Al-Aqsa Kabla ya Pasaka

9:37 - April 23, 2024
Habari ID: 3478720
IQNA - Makumi ya walowezi wa Kizayuni wamevamia Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) siku ya Jumatatu chini ya ulinzi mkali wa wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel ambao unakalia eneo hilo kwa mabavu.

Walowezi  172 walivamia msikiti mtakatifu wa Al Aqsa kwa kupitia  lango la Mughariba na kufanya ziara za uchochezi katika ua la msikiti huo. Pia walifanya matambiko ya Kiyahudi ya Talmudi

Wakati huohuo, wanajeshi wa utawala haramu wa Israeli waliokuwa na silaha nzito waliwalinda walowezi hao wa Kizayuni wakati wakiwa wanatekeleza uchochezi wao huo dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa kabla ya Pasaka ya Kiyahudi jana.

Makundi ya Walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali  yaliwataka wafuasi wao kufanya uvamizi mkubwa katika Msikiti wa Al-Aqsa usiku wa manane kabla ya Pasaka ya Kiyahudi ambayo imeanza jana 22 Aprili na inatazamiwa kuendelea hadi Aprili 30.

Vikundi vya Kizayuni vinavyojiita vya Harakati za Hekalu vimetoa wito kwa wafuasi wao kufanya uvamizi mkubwa katika Msikiti wa Al-Aqsa leo  ili kutoa "dhabihu,".

Mwaka huu, kikundi cha "Kurudi kwenye Mlima wa Hekalu" kilitoa zawadi za kifedha za hadi shekeli 50,000 (zaidi ya $ 13,000) kwa wale ambao wanaweza kufaulu kuchinja ndani ya boma la Al-Aqsa.

Duru za ndani zinasema kuwa, wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wamewaua Wapalestina 59 wa mji unaokaliwa kwa mabavu wa al-Quds na kuwajeruhi wengine karibu 172 tokea kuanza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Gaza Oktoba mwaka jana.

3488040

captcha