IQNA

Filamu ya 'Miujiza ya Qur'ani' kuonyeshwa nchini Uholanzi

11:47 - October 13, 2010
Habari ID: 2012091
Kamati ya Uenezi ya Taasisi ya Utamaduni ya al Kauthar ya Uholanzi imepanga kuonyesha filamu ya matukio ya kweli (documentary) ya Miujiza ya Qur'ani katika mji wa The Hague.
Filamu hiyo inaonyesha masuala ya kishangaza ya kisayansi ambayo Qur'ani Tukufu iliyazungumzia au kuyaashiria karne 14 zilizopita na wasomi wa zama hizo wamefanikiwa kufichua baadhi ya uhakika huo wa kisayansi kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Filamu hiyo imetengenezwa na Harun Yahya, mwandishi wa Uturuki anayesisitiza kuwa japokuwa Qur'ani Tukufu si kitabu cha sayansi lakini imezungumzia au kuashiria baadhi ya masuala ya kielimu ambayo yameelezwa katika aya nyingi kwa kutumia mbinu za fasihi na mantiki.
Mwandishi Harun Yahya anasema hakika za kielimu na kisayansi za Qur'ani hazikuwa katika fikra za mwanadamu wakati wa kuteremshwa kitabu hicho lakini wasomi wa zama hizi wamefanikia kueleza na kubainisha hakika hizo kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Ameongeza kuwa filamu ya Miujiza ya Qur'ani inaeleza kuwa kitabu hicho ni neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu lililoteremshwa kwa ajili ya kumwongoza mwanadamu na kumfikisha katika saada na ufanisi wa dunia na akhera. 674229

captcha