IQNA

Mawaziri wa Afya wa nchi za Kiislamu kukutana Kazakhstan

14:10 - September 26, 2011
Habari ID: 2193428
Mawaziri wa Afya wa nchi za Kiislamu wanatazamiwa kukutana huko Astana mji mkuu wa Kazakhstan tokea tarehe 29 Septemba hadi Mosi Oktoba.
Ekmeleddin Ihsanoglu Katika Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC anatazamiwa kuwasili mjini humo hapo kesho Jumanne baada ya kushiriki kwenye kikao maalumu cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kujadili na kupitishwa azimio la kubuniwa nchi mpya ya Palestina. Ihsanoghlu anatazamiwa kushiriki katika ufunguzi wa kikao hicho cha tatu cha Mawaziri wa Afya ambacho kinatazamiwa kuwajumuisha washiriki 400 kutoka nchi 57 wanachama wa OIC na baadhi ya mashirika ya kimataifa.
Katika hotuba yake kwenye kikao hicho, Ihsanoglu anatazamiwa kufafanua malengo ya kikao hicho. Lengo kuu la kuandaliwa kikao hicho limetajwa kuwa ni kuimarisha ushirikiano wa nchi wanachama wa OIC katika sekta ya afya na tiba.
Wawakilishi wa nchi tazamaji za OIC, mashirika yanayofungamana na jumuiya hiyo, mashirika ya kimataifa ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali, Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF na shirika la kimataifa la kupambana na Ukimwi ni miongoni mwa watu walioalikwa kushiriki kwenye kikao hicho cha Astana. 867258
captcha