IQNA

Moscow kuwa mji mkubwa zaidi wa Waislamu Ulaya

14:39 - July 22, 2015
Habari ID: 3332166
Ripoti zinaonyesha kuwa, idadi ya Waislamu katika mji mkuu wa Russia, Moscow inakuwa kwa haraka.

Utafiti uliofanywa na taasisi moja ya mjini Moscow inayoendeshwa na mwandishi mashuhuri, Ilya Varlamov, unaonyesha kuwa, mji wa Moscow unaelekea kuwa mji wenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya. Utafiti huo unaonyesha kuwa, idadi ya misikiti imeongezeka huku watu wanaosilimu wakiongezeka kila uchao. Waislamu wasiopungua milioni 1.5 walishiriki katika Sala ya Idul Fitr siku tatu zilizopita katika misikiti na maeneo mbalimbali mjini Moscow.

Licha ya kuenea chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya, lakini idadi ya waumini wa dini hiyo imekuwa ikiongezeka siku baada ya siku. Kwa sasa Ufaransa inahesabiwa kuwa nchi yenye Waislamu wengi zaidi barani Ulaya.../mh

3331924

Kishikizo: Moscow waislamu ulaya
captcha