IQNA

Mashindano ya 16 ya Qur'an Tukufu ya Russia Kufanyika

16:49 - September 12, 2015
Habari ID: 3361692
Awamu ya 16 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'an Tukufu ya Russia yanatazamiwa kufanyika kuanzia tarehe 19 Oktoba katika mji mkuu wa nchi hiyo, Moscow.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Moscow, mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'an Tukufu, yataanza tarehe 19 Oktoba mwaka huu katika ukumbi wa Crux City Hall mjini humo.
Hadi sasa idadi ya nchi zitakazoshiriki bado hawajatangazwa, ingawa maandalizi yanaendelea.
Mashindano ya Qur'an Tukufu hufanyika kila mwaka nchini Russia, chini ya usimamizi wa baraza la mamufti wa nchi hiyo kwa kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu na zisizo za Kiislamu.
Katika Awamu ya 16 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'an Tukufu ya Russia, kutakuwa na vitengo viwili vya kuhifadhi Qur'an na qiraa ya tajwidi. Kwa mujibu wa takwimu zisizo rasmi, Russia ina karibu Waislamu milioni 20 kati ya jamii yenye watu milioni 145 wa taifa hilo.

3361374

captcha