IQNA

Rais wa Iran asisitiza kuimarishwa uhusiano na Afrika Kusini

19:42 - April 24, 2016
Habari ID: 3470268
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuimarishwa uhusiano wa nchi hii na Afrika Kusini katika setka mbali mbali.

Rais Rouhani ameongeza kuwa  watu wa Iran walisimama bega kwa bega na kuwaunga mkono wazalendo wa Afrika Kusini wakati wakipambana na utawala wa makaburi wabaguzi wa rangi.

Rais Rouhani ameyasema hayo Jumapili mjini Tehran katika mkutano wa pamoja wa waandishi habari akiwa ameandamana na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini. Rais Rouhani ameitaja safari ya Zuma kuwa muhimu sana na kuongeza kuwa: "Katika safari ya Jacob Zuma Tehran, kutaimarisha uhusiano wa nchi mbili muhimu yaani Iran kama nchi yenye taathira katika eneo neyeti la Mashariki ya Kati na Afrika Kusini kama nchi muhimu barani Afrika."

Zuma amesisitiza kuwa, tokea ishike madaraka serikali ya chama cha ANC Afrika Kusini baada ya kuangusha mfumo wa ubaguzi wa rangi, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa na uhusiano mzuri na wa karibu na Afrika Kusini.
Rouhani ameongeza kuwa katika mazungumzo ya faragha na ya wazi na Jacob Zuma, pande mbiliz zimejadili kuhusu kutumia uwezo wa Iran na Afrika Kusini katika uga wa uchumi, biashara, sayansi, teknolojia na pia kuhusu masuala ya kieneo na kimataifa.
Rais wa Iran pia amesema Iran na Afrika Kusini zinaweza kuimarisha uhusiano katika sekta za benki ili kuimarisha uhusiano wa pande mbili.
Katika mkutano huo wa leo wa marais wa Iran na Afrika Kusini, nchi mbili zimetiliana saini mikataba nane kuhusu kuimarisha uhusiano katika sekta mbali mbali. Zuma aliwasili Tehran leo Jumapili akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa kisiasa na kiuchumi unajumuisha watu 180 kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa pande mbli.

Kwingineko Naibu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayeshughulikia masuala ya wanawake Bi. Shahindokht Molaverdi amesema Iran na Afrika Kusini zitashirikiana katika kuinua hadhi ya wanawake. 

Ameyasema hayo Jumapili mjini Tehran alipokutana na kufnaya mazungumzo na Bi. Bongi Ngema-Zuma mke wa rais wa Afrika Kusini aliye safarini nchini Iran.
Bi. Molaverdi amesema serikali ya Iran inalipam kipaumbele suala la ustawi wa uwezo wa wanawake na kuongeza kuwa: "Hivi sasa tunafuatilia suala la kuimarisha uwezo wa wanawake kote Iran na kwa hivyo kubadilishana mawazo na Afrika Kusini kuhusu suala hili kutatoa msaada mkubwa kwa wanawake."
Kwa upande wa Bi. Bongi Ngema-Zuma amesema wakati wanawake wanapokuwa na uwezoz taifa nalo hupata uwezo.
Aidha amesema serikali ya Afrika Kusini imechukua hatua za kuleta usawa wa kijinsia na kwamba baad aya kuangua mfumo wa ubaguzi wa rangi, wanawake Afrika Kusini wameshuhudia ustawi mkubwa.
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini aliwasili Tehran jana Jumapili akiongoza ujumbe wa watu 180 wakiwemo maafisa wa serikali na wawekezaji. Rais Zuma anatembelea Iran kufuatia mwaliko wa mwenyeji wake Rais Rouhani ili kujadili masuala ya kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika nyuga tofauti.
Marais hao jana walikutana katika Ikulu ya Saadabad, na kujadili masuala ya kuimarisha uhusiano wa pande mbili, mbali na kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kieneo na kimataifa.

3491652

captcha