IQNA

Waislamu wasiojiweza Uganda wapokea misaada ya futari

15:02 - June 16, 2016
Habari ID: 3470390
Huku Waislamu duniani wakiwa katika wiki ya pili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, shirika moja la kutoa misaada ya chakula cha futari kwa watu wasijiweza nchini Uganda.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Uganda (HEAR) limetoa misaada ya chakula chenye thamani ya takriabani dola 27,500 kwa ajili ya Waislamu wasiojiweza.

Mwenyekiti wa Shirika la Msaada la HEAR, Ahmad Sentami amesema wamepata ilhamu ya kutoa msaada kutoka kwa Mtume Muhammad SAW ambaye amesema mwenye kumsaidia mwenye kufunga kufuturu atapata thawabu za sawm za mwenye kufuturishwa bila thabai za mwenye kusaidiwa kupungua.

Sentamu amesema wanaofaidika ni misaada hiyo ni pamoja na wazee, wagonjwa, wajane, wenye ulemavu na wengine wasiojiweza.

3507317

captcha