IQNA

Mafunzo ya Kiislamu kwa Waislamu nchini Uganda

0:06 - August 07, 2016
Habari ID: 3470500
Kozi ya mafunzo ya Kiislamu katika kipindi cha muda mfupi imemamalizika hivi karibuni nchini Uganda kwa kutolewa zawadi kwa wanafunzi bora.

Kwa mujibu mwa mwandishi wa IQNA, mafunzo hayo ya Kiislamu yametolewa na Chuo cha Al Mustafa SAW nchini Uganda ambapo washiriki, wakiwemo wanaume na wanawake, wamepata mafunzo yenye lengo la kuongeza maarifa yao ya Kiislamu.

Katika kozi hiyo ya muda mfupi, wanafunzi wamejifunza sayansi za Qur’ani, tafsiri ya Qur’ani, historia ya Uislamu, kuijia Nahjul Balagah, Utamaduni wa Kiislamu, haki za wanawake na sira ya Bibi Fatima SAW na pia umuhimu wa familia katika Uislamu.

Ali Bakhtiari, Mkuuwa Kitengo cha Utamaduni cha Iran mjini Kampala, Uganda ametoa mafundisho maalumu kuhusu utamaduni wa Kiislamu.

Kozi hiyo fupi ilimalizika kwa wanafunzi bora kupata zawadi na cheti cha ushiriki kwa wote.

3520522

Kishikizo: qurani waislamu uganda iqna
captcha