IQNA

Mkutano wa Umoja wa Kiislamu kufanyika Moscow

20:41 - October 18, 2016
Habari ID: 3470619
Russia na Iran zinashirikiana katika kuandaa kongamano la Umoja wa Kiislamu mjini Moscow.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, konamani hilo linafanyika Jumatano 19 na limeandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu, yenye makao yake Tehran, kwa ushirikiano wa Baraza la Mamufti wa Russia.

Mkuu wa masuala ya kimataifa katika Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu Bw. Manoucher Mottaki amesema kongamano hilo linalenga kuimarisha umoja wa Kiislamu na kupinga idiolojia ya Kitakfiri na misimamo mikali ya kidini.

Amesema mkutano huo utahudhuriwa na wanazuoni, wasomi, na wanafikra kutoka nchi hizi mbili na nchi kadhaa za Kiislamu.

Ujumbe wa Iran katika kongamano hilo utaongozwa na Ayatullah Muhsin Araki, Katibu Mkuu Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu. Ujumbe huo unajumuisha wanazuoni wa Kishia na Kisunni kutoka maeneo mbali mbali ya Iran.

Bw. Mottaki amebaini kuwa, katika kipindi cha miaka mitano sasa, maadui wa Uislamu wamekuwa wakitumia makundi ya magaidi wakufurishaji kueneza vita vya ndani katika nchi za Kiislamu na maeneo mengine duniani. Aidha ametoa bishara njema na kusema makundi hayo ya kigaidi hivi sasa yanaelekeka kufika ukingoni.

3538749/

captcha