IQNA

Kongamano la Umoja wa Kiislamu Lafanyika Indonesia

21:18 - November 28, 2016
Habari ID: 3470702
Kongamano la Kimataifa la “Umoja wa Kiislamu, Dharura na Changamoto katika Mustakabali” linafanyika nchini Indonesia.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo ambalo linafanyika 29 Novemba mjini Jakarta limeandaliwa na Jumuiya ya Mahmudiya ya Indonesia kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu yenye makao yake mjini Tehran.

Kongamano hilo linahudhuriwa na maulamaa wa Kiislamu kutoka kote Indonesia na pia nchi za kieneo kama vile Ufilipino, Brunei, Thailand, Malaysia n.k. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu Ayatullah Muhsin Araki ni kati ya watakaohudhuria kikao hicho.

Mada muhimu zitakazojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na, ‘Umoja wa Kiislamu kama Faradhi ya Qur’ani na Sunna ya Mtume SAW’, ‘Mustakabali wa Umoja wa Kiislamu’, ‘Fitina za Kimadhehebu na tatizo la misimamo mikali na ukufurishaji’, ‘Kadhia ya Palestina na Jukumu letu la Kiislamu’.

Ayatullah Muhsin Araki anaongoza ujumbe wa ngazi za juu wa Iran katika kongamano hilo.

3549674

captcha