IQNA

Gazeti la Brunei lafungwa kwa kulalamikia Saudia kuongeza bei ya visa ya Hija

21:23 - November 09, 2016
Habari ID: 3470664
IQNA-Gazeti moja mashuhuri nchini Brunei limefungwa baada ya kuandika kuwa matatizo ya kiuchumi Saudi Arabia yameipelekea iongeze kwa kiasi kikubwa bei ya Visa ya Hija.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, gazeti la Brunei Times ambalo liko katika nchi hiyo ndogo ya kusini mashariki mwa Asia limefungwa baada ya kuandika tahariri iliyokosoa vikali Saudi Arabia.

Katika toleo lake la 26 Oktoba, gazeti hilo liliandika kuwa, matatizo ya kiuchumi Saudia ndio sababu kuu iliyoplekea wakuu wa Riyadh waongeze kwa kiasi kikubwa adha zinazolipwa kwa ajili ya Hija na Umrah katika mji mtakatifu wa Makka.

Katika taarifa, gazeti la Brunei Times limetaja sababu ya kusitisha uchapishaji kuwa ni changamoto za kikazi kutoka vyombo habari mbadala.

Hivi karibuni serikali ya Saudia iliongeza kwa asilimia 500 bei ya Visa kwa Waislamu wanaotaka kutekeleza ibada za Hija au Umrah . Katika nyongeza hiyo visa ya Hija ya kuingia mara moja sasa itahgairmu dola $ 533 kutoka dola $92 huku visa ya miezi sita ya kuingia mara kadhaa ikigharimu $800 na ile ya mwaka moja ikigharimu $1333.

Tayari mashirika ya usafiri katika nchi kadhaa yametangaza kusitisha safari za Umrah na Hija kutokana na nyongeza hiyo.

3461377

captcha