IQNA

Uislamu wazidi kuimarika nchini Zimbabwe

18:33 - November 15, 2016
Habari ID: 3470678
IQNA-Uislamu unazidi kuimarika na kuenea kote huko Zimbabwe kutokana watu wa nchi hiyo kutambua itikadi za dini hii tukufu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Jarida la African Exponent limechapisha makala maalumu inayosema kuwa Uislamu unaendelea kuwavutia Wazimbabwe. Mwandishi wa makala anasema sambamba na kuenezwa mafundisho ya Uislamu pia kuna wale wanaoeneza chuki dhidi ya Uislamu.

Zimbabwe ina idadi ya watu milioni 15 ambapo asilimia 2 ni Waislamu na ingawa idadi hiyo kidhahiri inaonekana duni, ni hatua kubwa katika nchi ambayo inafungamana sana na mafundisho ya Kikristo na itikadi za jadi.

Uislamu hutambuliwa na wengi Zimbabwe kama dini ya wageni lakini hivi sasa ni jambo la kawaida kuwaona Wazimbabwe wazalendo wakiwa wamevaa kanzu na kofia wakienda msikitini kwa ajili ya ibada au masomo ya Kiislamu.

a mujibu wa mwandishi wa IQNA, Jarida la African Exponent limechapisha makala maalumu inayosema kuwa Uislamu unaendelea kuwavutia Wazimbabwe. Mwandishi wa makala anasema sambamba na kuenezwa mafundisho ya Uislamu pia kuna wale wanaoeneza chuki dhidi ya Uislamu.

Zimbabwe ina idadi ya watu milioni 15 ambapo asilimia 2 ni Waislamu na ingawa idadi hiyo kidhahiri inaonekana duni, ni hatua kubwa katika nchi ambayo inafungamana sana na mafundisho ya Kikristo na itikadi za jadi.

Uislamu hutambuliwa na wengi Zimbabwe kama dini ya wageni lakini hivi sasa ni jambo la kawaida kuwaona Wazimbabwe wazalendo wakiwa wamevaa kanzu na kofia wakienda msikitini kwa ajili ya ibada au masomo ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa Sheikh Binali, katiba ya mwaka 2013 ya Zimbabwe imerahisisha kazi za kuutangaza Uislamu kwani Waislamu sasa wanaweza kuenda vijijini kuhubiri pasina kutajwa kuwa wageni kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Waislamu Zimbabwe, sawa na maeneo mengine duniani, wangali wanakabiliwa na changamoto za propaganda za vyombo vya habari ambavyo vinaeneza chuki dhidi ya Uislamu na kuinasibisha dini hii tukufu na ugaidi. Uislamu wazidi kuimarika nchini Zimbabwe

Waislamu wa Zimbabwe wakiwa msikitini

Pamoja na hayo kuna nuka chanya ambazo zinashuhudiwa Zimbabwe kama wakati mbinge wa Harare Terence Mukupe aliposema kuna uwezekano wa kushirikiana na Waislamu katika kujenga shule. Mbunge huyo ameonekana kufurahishwa na itikadi ya Waislamu ya kutoa sadaka kwa wasiojiweza katika jamii.

Kwa kuzingatia kuwa Malawi ina idadi kubwa ya Waislamu, hakuna shaka kuwa Uislamu pia utaenea katika maeneo mengine ya kusini mwa Afrika.

3545924

captcha