IQNA

Baadhi ya 'Vituo vya Kiislamu' Ulaya vinaunga mkono ISIS

18:54 - December 03, 2016
Habari ID: 3470713
IQNA-Mufti Mkuu wa Syria Sheikh Badreddin Hassoun amesema baadhi ya vituo vinavyojiita kuwa vya Kiislamu barani Ulaya vinaunga mkono kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.

IQNA-Mufti Mkuu wa Syria Sheikh Badreddin Hassoun amesema baadhi ya vituo vinavyojiita kuwa vya Kiislamu barani Ulaya vinaunga mkono kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.

Akizungumza mapema wiki hii wakati alipohutubia Bunge la Ireland mjini Dublin, Sheikh Hassoun alisema zaidi ya nchi 80 zimetuma magaidi 360,000 nchini Syria.

Ameongeza kuwa, Syria imepata hasara kubwa katika mapambano makali dhidi ya magaidi wanaolenga kuiharibu nchi hiyo.

Sheikh Hassoun aidha ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia kwa uungaji mkono wao kwa serikali halali ya Syria na watu wa nchi hiyo walio mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi.

Aidha amekosoa vikali vyombo vya habari kwa kupotosha ukweli wa mambo Syria huku akitoa wito kwa wanasiasa wa Ulaya kutembelea Damascus na kujionea kwa wenywe yanayojiri nchini humo.

Syria ilikumbwa na vita vya ndani tokea Machi 2011 baada ya makundi kadhaa ya magaidi wakufurishaji wa Kiwahhabi wanaopata himaya ya kigeni, hasa ISIS, kuvamia nchi hiyo na kukalia kwa mabavu baadhi ya maeneo.

Taarifa ya Kituo cha Utafiti wa Syria kinasema kuwa vita hivyo vimepelekea watu 470,000 kupoteza maisha huku wengine karibu milioni mbili wakijeruhiwa na nusu ya Wasyria wote ambao walikuwa milioni 23 wakilazmika kuwa wakimbizi ndani au nje ya nchi.

Serikali ya Syria inasema waungaji mkono wa magaidi Syria ni baadhi ya nchi za Magharibi hasa Marekani na waitifaki wao katika eneo hasa Saudi Arabia, Utawala haramu wa Israel, Uturuki na Qatar.

3461561

captcha