IQNA

Iran kuandaa Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

10:36 - May 02, 2017
Habari ID: 3470964
TEHRAN (IQNA)-Awamu ya 25 ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yataanza mjini hapa katika siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mkurugenzi wa maonyesho hayoa Abbas Nazarirad amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa, maoneysho hayo yataendelea kwa muda wa siku 18. Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu wa 2017 unatazamiwa kuanza tarehe 27 Mei.

Bw. Nazarirad amesema mwaka huu sawa na miaka iliyopita, Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran yatafanyika katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA.

Aidha amesema kuwa milango ya maonyesho hayo itakuwa wazi kila siku kuanzia saa 12 jioni hadi saa sita usiku.

Afisa huyo amedokeza kuwa, nanra ya maonyesho ya mwaka huu ni "Qur'ani, Maadili na Maisha" na kwamba kutakuwa na hafla kadhaa kuhusiana na mada hii. Aidha mwaka huu kutakuwa na maonyesho maalumu yenye anuani ya: "Robo Karne ya Harakati za Qur'ani" ambapo washiriki watabainishiwa mafanikio ya maonyesho hayo ya kimataifa ya Qur'ani katika kipindi cha miaka 25 iliyopita.

3462727

captcha