IQNA

Kenya ni kati ya nchi 22 katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani Tehran

11:08 - June 03, 2017
Habari ID: 3471005
TEHRAN (IQNA)-Zaidi ya nchi 20 zinashiriki katika Maonyesho ya 25 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran mwaka huu.

Mkuu wa kitengo cha kimataifa cha maonyesho hayo Abbas Nazarirad amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa maonyesho yam waka huu yana washiriki wa kigeni kutoka nchi kama vile Tunisia, Poland, Algeria, Kenya, Afghanistan, Bangladesh, India, Iraq na Senegal.

Amesema miongoni mwa washiriki wa kigeni wamo watafiti, wanazuoni, pamoja na wataalamu wa Qur’ani Tukufu na pia waandishi habari.

Maonyesho ya 25 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yalianza Jumatatu Alasiri katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini SA mjini Tehran.

Maonyesho hayo ya kimataifa yanahudhuriwa na taasisi 50 na pia kuna mashirika zaidi ya 297 ya uchapishaji ambapo kati ya mashirika hayo, 281 ni kutoka Iran na 16 ni ya kimataifa kutoka nchi kama vile Uturuki, Iraq, Lebanon na Syria.

Mkurugenzi wa maonyesho hayoa Abbas Nazarirad amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa, maoneysho hayo yataendelea kwa muda wa siku 18.

Kaulimbiu ya maonyesho ya mwaka huu ni "Qur'ani, Maadili na Maisha" na kwamba kutakuwa na hafla kadhaa kuhusiana na mada hii. Aidha mwaka huu kutakuwa na maonyesho maalumu yenye anuani ya: "Robo Karne ya Harakati za Qur'ani" ambapo washiriki watabainishiwa mafanikio ya maonyesho hayo ya kimataifa ya Qur'ani katika kipindi cha miaka 25 iliyopita.

3605657

captcha