IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alishukuru jeshi la IRGC

14:36 - April 22, 2020
Habari ID: 3472692
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe maalumu wa kulishukuru na kulipongeza utendaji kazi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sepah News, Brigedia Jenerali Mohammad Shirazi Mkuu wa Ofisi ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran amempigia simu Meja Jenerali Hussein Salami Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kumtumia ujumbe wa Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran, kwa munasaba wa siku ya kuasisisiwa IRGC.

Katika mazungumzo hayo ya simu,  Brigedia Jenerali Shirazi amesema, Ayatullah Khamenei amepongeza utendaji kazi na jitihada nzuri za IRGC. 

Tarehe 21 Aprili miaka 41 iliyopita Imam Khomeini (M.A) mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitoa amri ya kuundwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). Kwa mujibu wa amri hiyo, jukumu kuu la jeshi hilo ni kulinda Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya maadui wa ndani na nje.

3893340

captcha