IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Huduma kubwa zaidi ya Shahidi Soleimani ilikuwa ni kuhuisha kambi ya muqawama

8:21 - January 01, 2024
Habari ID: 3478124
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kupanuka kwa jina, kumbukumbu na sifa za shahidi Qassim Suleimani kunatokana na ikhlasi ya shahidi huyo.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema hayo leo alipokutana na familia ya shahidi Luteni Jenerali Qassim Suleimani na kusisitiza kwamba, jukumu muhimu na huduma iliyotolewa na shahidi huyu ilikuwa ni kuhuisha kambi ya muqawama na mapambano katika eneo la Asia Magharibi.

Ayatullah Khamenei ambaye amekutana na familia ya shahidi Qassim Suleimani kwa mnasaba wa kukaribia hauli na mwaka wa nne tangu kuawa shahidi amesisitiiza kuwa, muqawama wa Gaza wa takriban miezi mitatu unatokana na kuwepo kambi ya muqawama na kuongeza kwamba, shahidi Suleimani alifanya juhudi kubwa kwa ajili ya kuhuisha kambi ya muqawama na  aliitekeleza kazi hiyo kwa ikhlasi na hekima na maadili mema.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, kuna haja ya kuendelezwa juhudi za kuimarisha kambi ya muqawama.

Luteni Jenerali Qasem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC-SEPAH), ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kigaidi la jeshi vamizi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. Hujuma hiyo ilitekelezwa kwa amri ya rais wa wakati huo wa Marekani, Donald Trump.

4191056

Habari zinazohusiana
captcha