IQNA

Hatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Mabeberu wanalenga kuvuruga usalama duniani

22:06 - October 29, 2021
Habari ID: 3474488
TEHRAN (IQNA)- Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa, harakati zinazofanywa na mabeberu kwa sasa zinalenga kuvuruga amani na usalama.

Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Muhammad Hassan Abu Turabi Fard amesema katika hotuba za Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran kwamba kundi la Daesh ni mfano wa makundi yaliyoanzishwa na madola ya kibeberu ambayo yanazuia maslahi halali ya nchi mbalimbali hususan nchi za Waislamu. 

Hatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo ya Tehran ameongeza kuwa, mienendo ya mabeberu wa sasa inafanana na ile ya Muawiya bin Abi Sufiyan katika zama za utawala wa Imam Ali bin Abi Twalib AS na kwamba haina lengo jingine ghairi ya kuvuruga na kuchafua amani. 

Sayyid Abu Turabi Fard amesema kuwa suala la kuunda serikali na utawala ni miongoni mwa fikra za kidini na kuongeza kuwa, kuna ushahidi mwingi katika Qur'ani na sira na mienendo ya Mtume Muhammad SAW inayoonesha kuwa Mitume wa Mwenyezi Mungu hususan Mtume wa Mwisho Muhammad SAW walifanya jitihada za kuunda serikali na mfumo wa kisiasa kwa shabaha ya kunjenga mwanadamu kwa misingi ya uadilifu na jamii ya kiadilifu sambamba na kulea wanadamu waadilifu.

Hatibu wa Saala ya Ijumaa ya Tehran amesema Mitume na Mawalii wa Mwenyezi Mungu walianzisha mifumo ya kisiasa na utawala kwa ajili ya saada na ufanisi wa mwanadamu na kwamba ni muhali kuweza kutimiza malengo ya Mitume hao bila ya kuwepo mfumo wa kisiasa makini, athirifu na unaotegemea wahyi na ufunuo. 

4008802

captcha