IQNA

Hatibu wa Sala ya Ijumaa: Iran haitakubali mazungumzo yasiyo na mwelekeo

18:20 - November 05, 2021
Habari ID: 3474516
TEHRAN (IQNA)- Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa Iran iko tayari kuingia kwenye mazungumzo ambayo matokeo yake ni kuondolewa vikwazo vyote na kwamba haikubali mazungumzo yasiyo na mwelekeo.

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema katika hotuba za Swala ya Ijumaa ya leo ya Tehran kwamba nara ya "Mauti kwa Marekani" ni kaulimbiu tukufu la taifa la Iran kwa sababu nchi hiyo ina faili jeusi mbele ya Wairani na ilishirikiana na Sadda Hussein kuishambulia Iran.

Imamu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa, jaribio la la karibuni la kuiba mafuta ya Iran la jeshi la Marekani katika maji ya Bahari ya Oman ni mwendelezo wa uovu na uadui wa Marekani dhidi ya taifa la Iran na kwa sababu hiyo Wairani wanatoa nara ya "Mauti kwa Marekani."  

Ayatullah Ahmad Khatami amesema kuwa Wamarekani wanasubiri kwa hamu kubwa fursa ya kufanya mazungumzo na Iran na kuongeza kuwa: Tuko tayari kwa mazungumzo ambayo matokeo yake ni kufutwa vikwazo vyote, na Iran ya Kiislamu haikubali mazungumzo ya mmomonyoko na yasiyo na mwelekeo. 

Kuhusiana na baadhi ya nchi washirika katika jinai za Marekani na zinazotoa vitisho daima dhidi ya Iran, hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema: "Siasa za ujirani mwema na ustahamilivu zinapewa thamani kubwa katika dini yetu; tunawaambia majirani zetu kwamba Iran ni nguvu kubwa zaidi ya kijeshi katika kanda hii ya Magharibi mwa Asia na mnapaswa kuamiliana na jirani mzuri na mwenye nguvu kwa mienendo ya kidugu, la sivyo mtauona moshi kwa macho yenu wenyewe na mtatumbukia kisimani na kuangamia pamoja na utawala wa Kizayuni wa Israel."

4010750

captcha