IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah

Hali ya ndani na matukio ya kimataifa yanaashiria kuangamia Israel

14:35 - February 24, 2022
Habari ID: 3474968
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah amesema hali ya ndani ya utawala ghasibu wa Israel u na matukio ya kimataifa yote kwa pamoja yanaashiria kuangamia utawala huo katili.

Sayyid Hassan Nasrallah amesema hayo Jumatano katika hauli na kumbukumbu ya kuuawa shahidi Sayyid Abbas Musawi. Katibu Mkuu wa zamani wa Hizbullah ya Lebanon ambapo akiashiria kuhusiana na kuangamia utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel, Nasrallah ameelezea kwamba, kuhusiana na hilo mjadala ni zama na wakati tu, na kusisitiza kwamba, hali ya ndani ya utawala huo ghasibu na matukio ya kimataifa yote kwa pamoja yanaashiria kuangamia utawala huo katili.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, hii leo harakati ya muqawama ina nguvu kuliko wakati wowote ule na kwamba, lengo hasa la muqawama ni kupigania uadilifu, amani, kuunga mkono wananchi, kutetea uhuru, ardhi, umma na matukufu yake.

Aidha amesema kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyopata ushindi mwaka 1979 kwa uongozi wa Imam Ruhullah Khomeini (MA) ulikuwa ni muujiza.

Katibu Mkuu wa zamani wa Hizbullah ya Lebanon na kubainisha kwamba, Imam Khomeini akipata himaya ya wananchi alifanikiwa kusambaratisha utawala muovu na mbaya kabisa katika eneo la Mashariki ya Kati yaani utawala wa Shah na kuzitimua Marekani na utawala haramu wa Israel kutoka  nchini Iran.

Hassan Nasrallah amesisitiza kuwa, ushindi wa mapinduzi hayo ya Kiislamu ya Iran kwa hakika ilikuwa ni nembo ya muujiza.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameashiria huba na mapenzi makubwa ya shahidi Sayyid Abbas Musawi kwa Imam Khomeini na kueleza kwamba, kiongozi huyo wa zamani wa Hizbullah alikuwa bega kwa bega na Imam Khomeini wakati wa kujiri harakati za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

3477939

captcha