IQNA

Kiongozi wa Hizbullah

Nasrallah: Israel haijafikia malengo yoyote huko Gaza baada ya siku 100

7:25 - January 15, 2024
Habari ID: 3478199
IQNA-Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah amesema utawala haramu wa Israel mepata hasara "isiyo na kifani" mikononi mwa makundi ya Kiiislamu ya kupigania ukombozi wa Palestina (muqawama) na imeshindwa kufikia malengo yake yoyote baada ya siku 100 za vita vyake vya mauaji ya kimbari kwenye Ukanda wa Gaza.

Sayyed Hassan Nasrallah aliyasema hayo katika hotuba yake ya televisheni siku ya Jumapili katika khitma ya siku ya saba tokea auawe shahidi Wissam Hassan al-Tawil, kamanda mkuu wa Hizbullah aliyeuawa katika shambulizi la Israel katika kijiji cha Khirbet Selm kusini mwa Lebanon tarehe 8 Januari.

Nasrallah amemsifu Tawil kuwa ni mmoja wa makamanda katika vita dhidi ya kundi la kigaidi na kiktakfiri la Daesh i nchini Syria na kusisitiza kuwa yeye pia amekuwa mmoja wa makamanda wa eneo la kusini tangu tarehe 8 Oktoba 2023, wakati harakati ya muqawama ya Lebanon ilipofanya mabadilishano ya moto. na utawala ghasibu wa Israel ukiwaunga mkono Wapalestina huko Gaza.

Nasrallah ameangazia mapambano na muqawama wa Palestina dhidi ya uvamizi wa Israel baada ya siku 100 na kusema kuwa utawala huo ghasibu wa Israel haujafanikiwa kufikia malengo yoyote vita hivyo yawe ya wazi au ya siri.

Kiongozi wa Hizbullah ameongeza kuwa: "Siku mia moja zimepita na Gaza na watu wake wamebaki imara katika njia ambayo historia haijawahi kushuhudia."

Aidha amesema: "Malengo ya vita vya Israel ni kuikalia Gaza, kuwaondoa Wagaza na kugeuza eneo hilo kuwa ufuo wa walowezi wa Israel," aliongeza. "Adui Muisraeli hakuweza kuondoa wanamapambano huko Gaza, wala kuangamiza harakati ya Hamas."

Akisisitiza kwamba mapambano ya Lebanon yamekuwa wazi tangu Oktoba, Sayyid Nasrallah alionyesha utayari wa Hizbollah wa kupambana na kusema Lebanon haina hofu ya vita au vitisho vya Marekani na Israel.

Kiongozi wa Hizbullah amesema: "Wale ambao wanapaswa kuogopa vita ni Israeli na walowezi wake."

“Tumekuwa tayari kwa vita kwa siku 99 zilizopita na hatuhofii. Tutapambana bila vikwazo."

Akionya kwamba Wamarekani lazima wahofie vituo vyao vya kijeshi katika eneo la Asia Magharibi, Nasrallah alisema, "Msimamo wetu ni kwamba upande wa Lebanon umekuwa wa kuunga mkono na kuisaidia Gaza na lengo lake ni kusitisha vita dhidi ya Gaza.  

Nasrallah amesema muqawama unaendelea kuusababishia hasara utawala ghasibu wa Israel lakini utawala huo ghasibu umekuwa ukificha idadi halisi ya askari wake waliouawa au kujeruhiwa vitani.

Amesema janga kubwa zaidi litakuwa wakati vita vitakapomalizika na kufichuka kiwango cha maafa yaliyoikumba Israel mikononi mwa harakati za kupigania ukombozi wa Palestina huko Gaza.

4193913

Habari zinazohusiana
captcha