IQNA

Wanafunzi 700 wahitimu kuhifadhi Qur’ani nchini Ethiopia

10:42 - March 24, 2022
Habari ID: 3475071
TEHRAN (IQNA)- Huku Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ukikaribia, wanafunzi 700 wamehitimu somo la kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu ambapo wote waliofuzu watatumwa katika misikiti mbali mbali nchini humo.

Mahafali ya kuhitimu wanafunzi hao 700 imefanyika katika jimbo la Oromia katika Kituo cha Kiislamu cha Zayd Bin Thabit.

Mhubiri maarufu wa Ethiopia, Sheikjh Amin Ibro ameseambaza picha na klipu za mahafali hiyo ambapo wanafunzi wanafunzi wanaonekana wakiwa wanashiriki katika sherehe za kuhitimu kwao.

Waislamu ni karibu asilimia 35 ya watu wote milioni 110 nchini Ethiopia wakiafuatiwa na Wakristo wa Kiorthodoxi ambao ni takribani asilimia 40.

فارغ التحصیلی 700 حافظ قرآن در اتیوپی در آستانه ماه مبارک رمضان + فیلم  /// اماده

4044737/

captcha