IQNA

Hali ya Iraq

Serikali mpya yaundwa Iraq baada ya mzozo wa muda mrefu

20:08 - October 28, 2022
Habari ID: 3475998
TEHRAN (IQNA)- Bunge la Iraq limeipasisha serikali ya Waziri Mkuu Mohammad Shia al-Sudani baada ya kuipigia kura ya kuwa na imani nayo.

Kupasishwa serikali ya Waziri Mkuu huyo mpya kumehitimisha mkwamo wa kisiasa katika nchi hiyo uliodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Matumaini ya kufikia tamati mkwamo wa kisiasa nchini Iraq yalifufuka majuma mawili yaliyopita, baada Bunge la Iraq kumchagua Abdul Latif Rashid kuwa Rais mpya wan chi hiyo ambapo rais naye katika hatua yake ya awali alimteua Mohammed Shia al-Sudani kuwa Waziri Mkuu na kumpatia jukumu la kuunda serikali.

Abdul Latif Rashid alipata kura 162 na hivyo kufanikiwa kumuondoa katika duru ya mchuano Barhum Saleh aliyepata kura 99 baada ya kuhesabiwa kura zote zilizopigwa katika duru ya pili ya upigaji kura bungeni; na hivyo akawa rais mpya rasmi wa Iraq.

Serikali mpya ya Iraq chini ya Waziri Mkuu Mohammad Shia al-Sudani inakabiliwa na changamoto nyingi likiwemo suala la usalama na kuboresha uchumi ambao umezorota mno katika kipindi hiki cha mwaka mmoja cha mzozo wa kisiasa nchini humo.

Mataifa na shakhhsia mbalimbalii wa kieneo na kimataifa wametuma salamu za pongezi kwa Waziri Mkuu, Rais na wananchi wa Iraq kwa kuundwa serikali mpya na kuiondoa nchi hiyo katika mkwamo wa kisiasa.

Kupigiwa kura ya kuwa na imani na serikali ya Waziri Mkuu Mohammad Shia al-Sudani licha ya kuhesabiwa kuwa pigo kubwa kwa mrengo wa Sadr ambao katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ulikwamisha kwa vizuizi mbalimbali kuarifishwa Waziri Mkuu na kuundwa serikali huko Iraq, lakini kunaonyesha kupatikana umoja kati ya makundi ya kisiasa ya Iraq kwa ajili ya kuvuka mkwamo wa kisiasa ulioigubika nchi hiyo kwa muda mrefu.

3481022

 

captcha