IQNA

Qur'ani Tukufu

Mashindano ya Kimataifa ya Kusoma Qur'ani Tukufu kufanyika Iraq

18:04 - December 20, 2023
Habari ID: 3478064
IQNA – Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) inapanga kuandaa mashindano ya kila mwaka ya kusoma Qur'ani Tukufu.

Mashindano hayo yanayojulikana kama Hudan Lil Muttaqeen (mwongozo kwa wachamungu), yatahudhuriwa na wasomaji 80 wa Qur'ani Tukufu kutoka Iraq na nchi nyinginezo.

Jafar al-Mousawi, mkurugenzi wa Televisheni ya Qur'an yenye uhusiano na Mitandao ya Televisheni ya Satalaiti ya Karbala, alisema mashindano hayo yatafanyika kila mwaka kwa amri ya Sheikh Abdul Mahdi al-Karbalayi, mwakilishi wa Marja'iya na Idara ya  Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS).  Alisema waandaaji, wajumbe wa jopo la majaji, na wasimamizi wa shindano hilo watakuwa Wairaki.

Idara hiyo imetenga tuzo na zawadi za pesa taslimu kwa washindi wa shindano hilo, alibainisha. Al-Mousawi ameongeza kuwa kutakuwa na zawadi maalum kwa mshindi wa juu, yaani ataruhusiwa kupanda Ma’zaneh ya haram tukufu ya Imam Hussein (AS).

Ma’zaneh ni sehemu ya juu kabisa ya mnara ambapo muadhini husoma Adhana (mwito kwa maombi). Bado hakuna maneno kuhusu ni lini toleo la kwanza la tukio la Qur'ani litafanyika. Kumekuwa na mwelekeo unaokua wa programu za Qur'ani Tukufu kama vile mashindano, vipindi vya kisomo na programu za elimu zilizofanyika nchini katika miaka ya hivi karibuni.

4188887

captcha