IQNA

Malenga wa Kiislamu

Pakistan yamkumbuka Malenga Allama Iqbal Lahori aliyewaamsha Waislamu wa Bara Hindi

12:35 - November 10, 2022
Habari ID: 3476066
TEHRAN (IQNA) – Maadhimisho ya miaka 145 ya kuzaliwa kwa mshairi wa Pakistani Allama Muhammad Iqbal yaliadhimishwa kote nchini humo kwa hamasa ya kitaifa siku ya Jumatano.

Siku ilipambazuka kwa maombi maalum misikitini kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Pakistan. Aliyejulikana kama Mshairi wa Mashariki, Allama Muhammad Iqbal alizaliwa huko Sialkot mnamo Novemba 9, 1877. Alipata elimu yake ya awali katika chuo cha kidini na kisha akaenda  Shule ya Misheni ya Sialkot, kutoka ambapo alifaulu mitihani yake yake ya shule ya upili.

Alipata Shahada yake ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali, Lahore mnamo 1897 na kupata Shahada yake ya Uzamili miaka miwili baadaye.

Malengo huyu maarufu ambaye pia alikuwa maarufu kama Allama Iqbal Lahori aliteuliwa kuwa mhadhiri wa historia, falsafa na Kiingereza katika Chuo cha Mashariki cha Lahore.

Aliwaamsha Waislamu wa Bara Hindi kupitia mashairi yenye ufahamu wa kina na aliwasilisha wazo la kuundwa kwa Pakistan kupitia hotuba yake ya kihistoria huko Allahabad mnamo 1930.

Hotuba ya Allama Iqbal ilitoa mwelekeo wazi na utambulisho tofauti kwa Waislamu wa Bara Hindi kwa kuunda nchi ya Pakistan. Allamah Muhammad Iqbal alifariki dunia mwaka 1938.

3481193

captcha