IQNA

Uislamu Tanzania

Maonyesho ya Hijabu yafanyika nchini Tanzania

19:06 - January 16, 2023
Habari ID: 3476412
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Tanzania kimeandaa maonyesho ya Kiislamu ya Hijabu na Ifaf (staha).

Maonyesho hayo yameandaliwa  kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa Bibi Fatima Zahra (SA),  bintiye Mtume Muhammad (SAW).

Kwa mujibu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO), maonyesho hayo yanalenga kutambulisha bidhaa zinazohusiana na Hijabu na mtindo wa maisha wa Kiislamu.

Vitu mbalimbali vinavyohusiana na Hijabu na mavazi ya Kiislamu vinaonyeshwa kwenye maonyesho hayo.

Pia kuna mabango katika lugha ya Kiingereza yanayoeleza kuhusu Hijabu na staha na umuhimu wake katika Uislamu.

Halikadhalika kuna klipu zinaonyeshwa miongozo ya mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Khomeini (RA) na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei kuhusu umuhimu wa Hijabu.

Miongoni mwa wageni waliohudhuria maonyesho hayo ni wale waliohudhuria semina kuhusu "Nafasi ya Mama Katika Kuinua Kizazi Cha Watu Wema", ambayo pia iliandaliwa katika hafla hiyo wiki iliyopita.

Maonyesho ya Hijabu na Ifaf yataendeshwa katika Kituo cha Utamaduni cha Iran hadi Jumatano, Januari 18.

4115052

captcha