IQNA

Mfumo wa Kifedha wa Kiislamu

Benki ya KCB Tanzania yazindua Hatifungani ya kwanza ya Kiislamu yenye thamani ya dola milioni 4.4

20:41 - November 12, 2022
Habari ID: 3476075
TEHRAN (IQNA)- Benki ya KCB Tanzania imezindua Hatifungani (Dhamana za muda mrefu) yake ya kwanza ya Kiislamu yenye thamani ya Tsh10 bilioni ($4.4 milioni) kufadhili kitengo cha Sahl cha benki hiyo.

Hatifungani hiyo ya Kiislamu iliyopewa jina la KCB Fursa Sukuk ilizinduliwa mnamo Novemba 9 na itafungwa mnamo Desemba 5.

"KCB Fursa Sukuk inatoa fursa kwa Watanzania na wasio Watanzania, wauzaji reja reja, mashirika na taasisi kuwekeza katika soko la mitaji kwa miaka mitatu kwa mapato yanayotarajiwa ya asilimia 8.75 kwa mwaka, kila robo mwaka," Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Cosmas Kimaro alisema katika taarifa.

Kiwango cha chini cha uwekezaji wa uanzishaji kimewekwa kuwa Tsh500,000 (kama $218).

Benki itaorodhesha Hatu fungani  Soko la Hisa la Dar es Salaam baada ya ofa inayoendelea ya awali ya umma.

KCB inaungana na Benki ya NMB na Benki ya Taifa ya Biashara katika kutoa dhamana za muda mrefu mwaka huu.

NMB iliwasilisha dhamana ya muda mrefu ya Tsh25 bilioni (dola milioni 10.9) ya Jasiri  kwa lengo la kufadhili biashara zinazoongozwa na wanawake, huku Hatifungani ya NBC ya Twiga ikilenga kukusanya Tsh300 bilioni ($131 milioni) kwa ajili ya kufadhili biashara ndogo na za kati.

4098906

captcha