IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Aliyeivunjia heshima Qur'ani Tukufu Uswidi akamatwe na afikishwe katika mahakama za nchi za Kiislamu

21:36 - July 22, 2023
Habari ID: 3477321
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kutovukiwa adabu matukufu ya Waislamu hasa Qur'ani Tukufu huko nchini Uswidi ni tukio chungu na ni njama hatari sana akisisitiza kuwa, aliyefanya jinai hiyo lazima aadhibiwe, na maulamaa wote wa Kiislamu wanaafikiana katika hilo.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo katika ujumbe maalumu wa maandishi na kuongeza kuwa, serikali ya Uswidi ina wajibu wa kumtia mbaroni aliyefanya jinai hiyo na kumkabidhi kwa idara za mahakama za nchi za Waislamu. 

Sehemu moja ya ujumbe huo muhimu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu inasema: Serikali ya Uswidi inapaswa kuelewa kwamba, hatua yake ya kuunga mkono vitendo vya jinai imeifanya itangaze vita na Ulimwengu wa Kiislamu na ijipalilie chuki na uadui kutoka kwa kila Muislamu na serikali nyingi za Waislamu duniani. 

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, jukumu la serikali ya Uswidi ni kumtia mbaroni aliyetenda jinai hiyo na kumkabidhi kwa mahakama za nchi za Waislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha amesisitiza kuwa, wanaofanya njama hizo nyuma ya pazia nao wanapaswa kuelewa kuwa, Qur'ani Tukufu inaendelea kunawiri siku baada ya siku na nuru yake itazidi kung'ara na kwamba njama na vitendo kama hivyo ni dhalili mno kuweza kuzuia kuenea nuru ya Qur'ani kwenye nyoyo za walimwengu.

Katika upande mwingine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu haitaruhusu balozi mpya wa Uswidi kuja humu nchini kufuatia kuvunjiwa tena heshima Qur'ani Tukufu katika nchi hiyo ya Scandinavia, jinai ambayo ni ya pili yla aina hiyo kufanywa nchini Uswidikatika kipindi cha chini ya mwezi mmoja.

Amir-Abdollahian alisema hayo jana usiku katika mahojiano na Kanali ya Kwanza ya televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuongeza kuwa, ameagizwa na Rais Ebrahim Raisi kutoruhusu balozi mpya wa Uswidi kukanyaga ardhi ya Iran hadi pale serikali ya nchi hiyo itakapochukua hatua madhubuti za kukabiliana na ukiukaji unaoendelea wa kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu.

Kwa upande wake,  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf amesema leo Jumamosi wakati wa ufunguzi wa kikao cha wazi cha Bunge kwamba, serikali ya Uswidi si mkweli katika madai yake kuwa inapinga kuvunjiwa heshima matukufu ya Qur'ani kwani haijachukua hatua yoyote ya maana ya kuzuia kutokea tena vitendo kama hivyo.

3484444

captcha