IQNA

Shujaa

Islam, mvulana mwenye umri wa miaka 15 aliokoa maisha ya zaidi ya watu 100 wakati wa hujuma ya kigaidi Moscow

18:30 - March 25, 2024
Habari ID: 3478573
IQNA - Mvulana mwenye umri wa miaka 15 anayeitwa Islam amesifiwa baada ya kuokoa zaidi ya watu 100 wakati wa shambulio la kigaidi kwenye ukumbi wa tamasha mjini Moscow siku ya Ijumaa.

Islam Khalilov alikuwa kazini katika kazi yake ya muda kama mhudumu wa chumba cha nguo katika ukumbi wa Crocus City Hall wakati mashambulizi ya kigaidi yalipoanza.

Baada ya kusikia milio ya risasi, Islam aliwasaidia watu kupata njia ya kutokea kwa dharura na kuwaongoza zaidi ya watu 100 kutoroka, na kuwasaidia kutoka na hivyo kunusuru maisha yao.

Kufuatia kitendo hicho cha kishujaa, Idara ya Dini ya Kiislamu na Baraza la Mufti la Russia imemtunuku tuzo ya ushujaa.

Watu wenye silaha waliojificha walifyatua risasi kwenye Ukumbi wa Crocus uliojaa watu katika eneo la Krasnogorsk kaskazini Moscow cha Ijumaa jioni kabla ya tamasha la shambulio baya zaidi nchini Russia kwa angalau muongo mmoja.

Idara ya usalama ya Russia FSB ilisema watu 11 wamezuiliwa, wakiwemo watu wanne waliohusika moja kwa moja katika shambulio hilo huku idadi ya waliouawa ikiongezeka hadi takriban 150.

Kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) limedai kuhusika na hujuma hiyo ya kigaidi ambayo inaendelea kulaaniwa duniani kote.

Video iliyosambaa mitandaoni inaonyesha watu wanne waliojizatiti kwa bunduki ya otomatiki wakiwamiminia risasi watu waliokuwa wamekusanyika kwenye ukumbi wa tamasha kwenye viunga vya mji wa Moscow, dakika dakika chache baada ya kujiri mripuko na moto mkubwa kusambaa ukumbini hapo.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump katika kampeni zake za kuwania urais aliwahi kusema kuwa kundi la kigaidi la Daesh liliasisiwa na rais wa zamani wa nchi hiyo Barack Obama. Kundi hilo limehusika na vitendo vya kigaidi na kuua maelfu ya watu wasio na hatia duniani kote. Serikali ya Russia imekuwa mstari wa mbele kupambana na magaidi wa Daesh nchini Syria na imeweza kufanikiwa kuwaangamiza magaidi hao katika nchi hiyo ya Kiarabu.

 

 

 

 

 
 

3487709

Kishikizo: Moscow isis daesh kigaidi
captcha