IQNA

Kiongozi Muadhamu:Tunapinga uingiliaji wa Marekani nchini Iraq

12:20 - June 23, 2014
Habari ID: 1421482
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga uingiliaji wa Marekani na madola mengine katika masuala ya ndani ya Iraq.

Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema hayo Jumapili wakati alipoonana na mkuu na maafisa wa ngazi za juu wa Idara ya Mahakama ya Iran na kuongeza kuwa, Tehran inaamini kwamba wananchi, serikali na maraji'i wa kidini wa Iraq wanao uwezo wa kukomesha mashambulizi ya makundi ya kitakfiri nchini mwao.
Ameongeza kuwa, madola ya kibeberu yakiongozwa na Marekani ndiyo yaliyoko nyuma ya pazia la fitna na mashambulizi yanayoendelea Iraq hivi sasa na lengo lao kubwa ni kuwanyima wananchi wa nchi hiyo faida wa kuendelea kuwa na demokrasia inayowawezesha kujiamulia wenyewe mambo yao bila ya uingiliaji wa Marekani.
Ayatullahil Udhma Khamenei ameongeza kuwa, Marekani haikufurahishwa na uchaguzi na kujitokeza vizuri wananchi wa Iraq katika uchaguzi huo pamoja na hatua ya wananchi hao ya kutumia haki yao ya kuchagua viongozi wanaowapenda, kwani inataka kuwaweka madarakani watu ambao ni vibaraka wake huko Iraq.

1421131

Kishikizo: iraq khamenei
captcha