IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya Haram ya Hadhrat Abbbas (AS)

15:12 - February 03, 2024
Habari ID: 3478296
IQNA – Haram Takatifu ya Hadhrat Abbas (AS) katika mji wa Karbala nchini Iraq imetangaza tukio lake kubwa la Qur'ani, "Tuzo ya Kimataifa ya Al-Ameed ya Kuhifadhi Qur'ani," ambayo itafanyika kama mashindano ya televisheni yaliyo wazi kwa wasomaji kutoka nchi zote.

Mashindano hayo yanalenga kueneza mafundisho Qur'ani Tukufu na usomaji wake na kuonyesha vipaji na ujuzi wa washiriki.

Kulingana na tangazo lililotolewa kwa IQNA, wale wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo lazima wafuate masharti haya ya jumla:

  • Tuma video ya kisomo chako, ukichagua aya zozote za Qur'ani Tukufu, na muda usiozidi dakika tatu.
  • Ukubwa wa video usizidi mb 150.
  • Video inapaswa kuambatanishwa na maelezo yafuatayo: jina la mshiriki kama linavyoonekana kwenye pasipoti yake, nchi, umri, picha ya pasipoti iliyo wazi na picha rasmi ya kibinafsi.
  • Video lazima isiwe na sauti au athari zozote za kuona, vinginevyo mshiriki ataondolewa.
  • Video inapaswa kuwa ya karibuni na isiyohaririwa, na mshiriki ataje jina lake mwanzoni.
  • Kamera inapaswa kuwekwa si zaidi ya mita 2 kutoka kwa mshiriki, na video ichukuliwe kwa mlalo (horizontal) na iwe mwanga mzuri.
  • Washiriki walio na umri wa chini ya miaka 18 wanaweza kuleta mtu mmoja anayeandamana nao ikiwa atakubaliwa.
  • Int’l Quran Recitation Competition Announced Hazrat Abbas Holy Shrine

Ili kujiandikisha kwa shindano, washiriki wanapaswa kutuma video zao na taarifa zinazohitajika kwa akaunti ya shindano kwenye programu ya Telegram. Ikiwa wanakabiliwa na tatizo lolote kwa kutumia Telegram, wanaweza kutuma ujumbe kwa akaunti ya WhatsApp ya usaidizi kwa nambari: +9647760005311.

Kipindi cha kujiandikisha kitaanza Februari 3, 2024 na kumalizika Februari 16, 2024. Matokeo ya washiriki waliokubaliwa yatatangazwa Februari 17, 2024.

captcha