IQNA

Sayyed Nasrallah asisitiza kuungwa mkono mapamabno ya Wapalestina

20:48 - May 16, 2016
Habari ID: 3470315
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuhusu kuendelea kuunga mkono mapambano ya taifa linalodhulumiwa la Palestina katika makabiliano yake na utawala ghasibu wa Israel unaokalia Quds Tukufu kwa mabavu.

Sayyed Hassan Nasrallah amesema hayo katika ujumbe wake kwa Kongamano la Kimataifa la Kushikamana na al Aqsa ambalo limefanyika hapa Tehran Jumapili. Katika ujumbe huo ambao umesomwa na Sheikh Ali Damoush Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Hizbullah, Sayyed Nasrullah amesisitiza kuhusu kuwaunga mkono Wapalestina kwa njia zote.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ameongeza kuwa umma wa Kiislamu una majukumu mapya kuhusu yale yanayojiri katika Masjidul Aqsa. Sayyed Nasrallah amesema, "Israel si natija ya mradi wa Uayuni bali ni natija ya irada ya madola makubwa duniani."

Katika ujumbe wake huo, kiongozi wa Hizbullah amesisitiza kuwa tatizo la Palestina si kukabiliana na Israel kwani Israel inatumiwa na madola makubwa ya kiistikbari na mabeberu wa zamani na wa sasa duniani. Ameongeza kuwa Israel kimsingi ni kituo cha kijeshi cha madola ya Magharibi katika eneo. Katibu Mkuu wa Hizbullah katika ujumbe wake, ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuandaa Kongamano la Kimataifa la Kutangaza Mshikmanao na al Aqsa.

Kongamano hillo limehudhuriwa na vongozi wa ngazi za juu wa Iran na pia wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Asasi Zisizo za Kiserikali Zinazounga Mkono Palestina.

3459825

captcha