IQNA

Sayyid Hassan Nasrallah

Vita vya Syria si vya Shia na Sunni, Saudi Arabia inazuia ukombozi wa Palestina

17:46 - June 14, 2016
Habari ID: 3470386
Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah amesema Saudi Arabia sasa imekuwa kizingiti kikubwa katika ukombozi wa Palestina.

Akizungumza hivi karibuni wakati alipokutana na wapiganaji wa Harakati ya Hizbullah, Nasrallah amekosoa sera za Saudi katika eneo ambazo zimepelekea Wapalestina wakumbane na vizingiti katika harakati za kuizikomboa ardhi zao. Itakumbukw akuwa katika miezi ya hivi karibuni kumefichuka uhusiano wa siri kati ya utawala wa Saudia na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwingineko katika matamshi yake, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ameashiria kuhusika harakati hiyo katika vita nchini Syria dhidi ya magaidi Wakufurishaji na kusema, magaidi hao hawatambui mipaka.

Aidha amesisitiza kuwa, kinyume na baadhi wanavyodai, mgogoro wa sasa nchini Syria si baina ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni.

Kiongozi wa Hizbullah pia ameikosoa Uturuki kwa kuhusika na uchochezo wa vita nchini Syria na amebainia kuwa Ankara imefeli kufikia malengo yake katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Magaidi wanaopata himaya ya kigeni walianzisha vita dhidi ya Syria mwaka 2011. Serikali ya Syria inasema baadhi ya nchi za Magharibi na waitifaki woa katika eneo hasa Uturuki, Saudi Arabia, Qatar na Utawala haramu wa Israel ndio waungaji mkono wakuu wa makundi ya kigaidi kama vile ISIS au Daesh na Jabhatu Nusra.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu karibu nusu milioni wammeuawa vitani Syria huku karibu nusu ya watu wote milioni 23 wa nchi hiyo wakikimbia makazi yao.

3506815

captcha