IQNA

Kiongozi Muadhamu:

Sala na Kusoma Qur'ani Humkurubisha Mja kwa Mwenyezi Mungu

13:00 - December 14, 2016
Habari ID: 3470741
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, njia bora kabisa ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu ni kushikamana na Sala na kusoma Quráni.
Sala na Kusoma Qur'ani Humkurubisha Mja kwa Mwenyezi Mungu

Ayatullahil Udhma Sayyed Ali Khamenei ameongeza kuwa, tunapozingatia kwamba mtu huwa anazungumza moja kwa moja na Mwenyezi Mungu Mtukufu na Muweza wakati wa Sala, tutaona kuwa ibada hiyo humtunukia mja nguvu za kutawakali kwa Allah, ushujaa na kujiamini. Kwa msingi huo ametoa wito kwa vijana kudumisha Sala ya mwanzo wa wakati wake sambamba na kuitekeleza ibada hiyo kwa mazingationa pia kushikamana na kusoma Quráni na kuzingatia maana na uongofu uliomo ndani yake yake ili kujikurubisha zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Ayatullah Khamenei aliyasema hayo jana mjini Tehran wakati akihutubia sherehe za kubaleghe na kubeba majukumu ya kidini za wanafunzi elfu mbili wa kiume wa Shule za Msingi za mkoa wa Tehran na kuongeza kuwa, mabarobaro ambao ni watoto wa taifa la Iran leo hii, kesho watakuwa watu wazima na viongozi wa nchi, hivyo wana jukumu la kushiriki vilivyo katika minasaba na mijumuiko mbalimbali ili kujiwekea kinga ya njama kama hizo za adui.

Kwingineko katika hotuba yake, Kiongoziz Muadhamu alisema moja ya malengo makuu ya adui ni kujipenyeza kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni nchini Iran na anawalenga zaidi vijana na mabarobaro wa taifa hili la Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha amesema, kipindi cha kubaleghe mtu ni wakati muhimu sana ambao inabidi utumiwe vizuri kumfanya kijana abaleghe kimaanawi na kuongeza kuwa, siri ya maendeleo ya mtu binafsi na ya kijamii ni kulindwa uhusiano baina ya mtu huyo na Mwenyezi Mungu na kwamba kosa kubwa linalofanywa na ustaarabu wa Magharibi ambao hivi sasa unazidi kutoweka na kusambaratika, ni kujiweka kwake mbali na Mwenyezi Mungu.

Ayatullahil Udhma Khamenei amewataka vijana na mabarobaro kuwafanya mashahidi wa njia ya haki kuwa kigezo chao na kuwakumbusha kwa kuwaambia: Vijana wetu wengi azizi waliouawa kwenye njia ya kulinda uhuru wa taifa lao na maslahi ya nchi yao kwa lengo la kuondoa shari ya maadui, walijitolea kitu azizi na chenye thamani kubwa zaidi kwao, yaani nafsi na roho zao katika njia ya Mwenyezi Mungu.

3553720

captcha