IQNA

Maonyesho ya Qur'ani Tukufu

Mapendekezo yakaribishwa kuhusu Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran

15:11 - November 29, 2023
Habari ID: 3477962
TEHRAN (IQNA) - Waandaaji wa toleo lijalo la Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran wanakaribisha mawazo mapya ya kuandaa vyema tukio hilo la Qur'ani.

Idara ya Masuala ya Qur'ani na Etrat katika  Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu ya Iran imetoa mwito wa kuwasilishwa mawazo mapya kwa ajili ya maonyesho yajayo ambayo yatakuwa ya 31.

Imewaalika wataalamu na wengine kutoa mawazo na mapendekezo yao ya kuboresha maonyesho kwa njia mbalimbali.

Wanaotaka kutuma mapendekezo wana  hadi Januari 5, 2024, kuwasilisha mapendekezo yao kupitia tovuti www.iqfa.ir.

Mawazo yaliyopokelewa yatachambuliwa na kutathminiwa na yale bora zaidi ambayo yanaonekana kuwa yanawezekana na ambayo yangechangia uboreshaji wa maonyesho yatachaguliwa kwa utekelezaji.

Pia, wale ambao wametoa mawazo yaliyochaguliwa watatunukiwa.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza dhana za Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani.

Maonyesho hayo huwasilisha mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani nchini humo na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

4184580

Habari zinazohusiana
captcha