IQNA

Sayyid Nasrallah: Sheikh Ahmad Zein daima alikuwa akitetea mapambano ya Wapalestina

18:09 - April 01, 2021
Habari ID: 3473776
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema marhum Sheikh Ahmad Zein daima alikuwa akitetea mapambano ya Wapalestina na kupinga njama zote zilizolenga matukufu ya taifa hilo.

Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Hizbullah aliyasema hayo jioni ya jana katika hotuba yake mjini Betrirut kwenye kumbukumbu ya Sheikh Ahmad Zein aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maulama wa Kiislamu nchini Lebanon.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa, kambi ya Muqawama na mapambano ya Kiislamu imevuka kipindi kigumu na hatari zaidi cha historia yake na kuchukua hatua kali dhidi ya vitisho sambaba na kuimarisha uwezo wake. Amesema Waisraeli wana wasiwasi kutokana na kuongezeka nguvu na uwezo wa harakati ya Hizbullah na kwamba wanatishia kuanzisha vita huku wakiviogopa.

Kuhusu mazungumzo ya amani nchini Yemen, Sayyid Hassan Nasrullah amesema, vyombo vya habari vya mabeberu vinafanya jitihada za kusambaza habari za uongo kwa maslahi ya Saudi Arabia vikidai kwamba Wasaudia wanataka amani na suluhu lakini harakati ya Ansarullah ya Yemen inapinga amani. Amesema kuwa, kile kinachodaiwa ni mpango mpya wa amani wa Wasaudia kwa ajili ya kukomesha vita nchini Yemen ni vita mpya ya vyombo vya habari dhidi ya Yemen.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema vita vya Yemen havina mfungamano wowote na Shia wala Suni bali vilianzishwa kwa ajili ya kuhudumia malengo ya Marekani na mipango yake katika eneo la Magharibi mwa Asia. Amesema silaha iliyobakia katika mikono ya Wamarekani na Wazayuni ni kuanzisha fitina na vita vya kimadhehebu.    

Sheikh Ahmad al Zein aliyeaga dunia Machi 3 alikuwa mwanaharakati mkubwa wa kupigania ukombozi wa Palestina na kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo hili. Alikuwa anaamini kuwa, muqawama ndiyo njia pekee ya kuweza kuikomboa Quds na Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Msikiti wa al Aqsa. Alikumbana na matatizo mengi kutoka kwa Wazayuni katika mapambano yake hayo kama vile majaribio ya kumuua kigaidi, kumuudhi na kumuwekea vizingiti katika harakati zake.

 

3961938

captcha