Shambulio hilo, katika eneo la Al-Rashad karibu kilomita 65 (maili 40) kusini mwa mji wa Kirkuk, lilitokea baada tu ya saa sita usiku, afisa mwandamizi wa polisi wa Iraq amewaambia waandishi habari.
"Wanachama wa Daesh walilenga kizuizi cha polisi," alisema afisa huyo, ambaye hakutaka kutajwa jina.
"Kumi na tatu waliuawa na watatu walijeruhiwa" kati ya vikosi vya usalama, afisa huyo aliongeza.
Chanzo cha matibabu kilichoko Kirkuk kilithibitisha kujiri hujuma huo. Hakukuwa na madai ya mara moja ya uwajibikaji.
Daesh iliwahi kuteka maeneo makubwa ya Iraq mnamo 2014, kabla kutimuliwa katika kampeni ya kupambana na uasi.
Serikali ya Iraq ilitangaza rasmi kushindwa kundi hilo la kigaidi mwishoni mwa 2017, lakini mabaki ya kundi hilo hutekeleza mashamb ulizi ya kuvizia amra kwa mara kote Iraq.
Magaidi hulenga mara kwa mara jeshi la polisi na polisi kaskazini mwa Iraq, lakini shambulio hili lilikuwa moja wapo ya hatari zaidi mwaka huu.
Mwezi Julai pia hujuma ya bomu iliyodaiwa na Daesh iliwaua watu 30 katika soko la Al-Woheilat katika kitongoji cha Sadr, mjini Baghdad.