IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Mus'haf Mashhad, ni nakala kamili zaidi ya maandishi ya Kikufi ya Hijaz

15:03 - March 22, 2024
Habari ID: 3478554
IQNA - Kuna maandishi mengi ya Qur'ani Tukufu yanayohifadhiwa kwenye Maktaba ya Astan Quds Razavi mjini Mashhad, nchini Iran, ukiwemo Mus'haf Mashhad ambao umetajwa ni nakala kamili zaidi katika maandishi ya Kikufi ya Hijaz.

Haya ni kwa mujibu wa mtafiti na mfasiri wa Qur'ani Morteza Kariminia, akizungumza katika kongamano la wataalamu lililofanyika katika Maonyesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani Tehran Alhamisi jioni.

Alisema Msahafu huo  kurasa 252 umekuwa ukiwavutia wataalam tangu karibu miaka 100 iliyopita.

Ukilinganishwa na nakala zingine ambazo nyingi si kamili na zinajumuisha kurasa chache, hii ndiyo nakala kamili zaidi ya karne ya kwanza ya Hijri ambayo inapatikana, aliongeza.

Akizungumzia majaribio ya nchi za Magharibi yaliyolenga kuleta upotoshaji wa kihistoria na mashaka juu ya Qur'ani Tukufu, alisema Mus'haf Mashhad, umethibitishwa, kupitia mbinu za kitaalamu kama vile miadi ya radiocarbon, kuwa unmebainika kuwa wa zama zai karibu na Bi'that (uteuzi. Muhammad (SAW) kuwa Mtume, nukta ambayo imesambaratisha majaribio hayo ya Wamagharibi na kuondoa shaka miongoni mwa baadhi ya watu kuhusuana na maandishi ya Qur'ani Tukufu

Amesisitiza kwamba Mus'haf Mashhad una thamani na hadhi maalum miongoni mwa Misahafu mingono katika maktaba ya Astan Quds Razavi.

Seyed Ali Sarabi alikuwa mtaalamu mwingine wa Qur'ani Tukufu aliyezungumza katika kongamano hilo.

Amesema kulinda na kuhifadhi Misahafu ni jambo ambalo limesisitizwa na Maimamu Maasumin (AS).

Vile vile amepongeza juhudi zinazofanywa na Astan Quds Razavi za kukusanya na kuhifadhi nakala za maandishi ya zamani ya Qur'ani na vitabu vingine vya kidini na kutambulisha turathi hizo za Kiislamu kwa ulimwengu wa Kiislamu.

Maonyesho ya 31 Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yalizinduliwa rasmi katika hafla ya Jumatano jioni, tarehe 20 Machi.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza dhana za Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani nchini Iran na duniani.

Inaonyesha mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani nchini humo na pia bidhaa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili ya kutangaza Kitabu hicho Kitakatifu.

4206651

 

Habari zinazohusiana
captcha