IQNA

Sayyed Hassan Nasrallah

Hizbullah ingesubiri Waarabu Lebanon ingekuwa imekaliwa na Israel

15:25 - March 07, 2016
Habari ID: 3470184
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, lau kama tungelikaa na kusubiri stratijia na mikakati ya Umoja wa Waarabu, basi leo hii Israel ingelikuwa iko nchini Lebanon.

Sayyid Hassan Nasrullah amesema hayo Jumapili katika hafla ya kumuenzi shahid Ali Fayyadh (Alhaj Alaa) na kubainisha kuwa, lau usingelikuwepo muqawama wa Waislamu wa Kishia basi leo hii Lebanon ingelikuwa inatawaliwa na Israel, kungelikuwa na makoloni huko Lebanon na vijana wa Kilebanoni wangelikuwa wamejaa kwenye jela za Wazayuni hivi sasa.

Amesisitiza kuwa, chaguo letu kwa ajili ya kukomboa ardhi yetu lilikuwa ni muqawama na litaendelea kuwa muqawama na lau tungelikaa kimya basi ardhi yote ya Lebanon ingelikuwa sawa na ya mashamba ya Shaba'a yanayoendelea kukaliwa kwa mabavu na Israel.

Amesema, hapa ndipo inapoonekana faida na umuhimu wa uungaji mkono wa Syria na Iran kwa muqawama wa wananchi wa Lebanon.

Sayyid Hassan Nasrullah ameendelea kusema: Wale wanaotutuhumu kuwa muqawama wetu ni wa kimadhehebu, wanapaswa kujiuliza, tulipowaunga mkono Waislamu wa Bosnia, tuliwaunga mkono kwa kuwa ni Mashia? Waislamu wa Bosnia ni Ahlusunna Waljamaa, lakini tuliwaunga mkono.

Vile vile amehoji akisema, tawala za Waarabu zimefanya nini tangu mwaka 1967 hadi leo, je, zimeikomboa Masjidul Aqsa, Kibla cha Kwanza cha Waislamu kutoka katika makucha ya Wazayuni?

3459281

captcha