IQNA

SayyidHassan Nasrullah

Saudia inaongoza njama dhidi ya mapambano ya Kiislamu

22:31 - May 06, 2016
Habari ID: 3470296
Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya nchini Lebanon Hizbullah amesema utawala wa Saudi Arabia unatekeleza njama dhidi ya mapambano ya Kiislamu katika eneo.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya nchini Lebanon Hizbullah Sayyid Hassan Nasrullah ameongeza kuwa, ushindi wa muqawama au mapambano ya Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati utaendelea daima.

Sayyid Hassan ameyasema hayo leo jioni huko mjini Bairut, Lebanon katika sherehe za kuunga mkono harakati za mapambano ya Kiislamu ambapo sambamba na kutoa shukurani zake za dhati kwa pande ambazo zimekuwa zikiunga mkono harakati hizo za muqawama amesema kuwa, harakati ya mapambano kwa ajili ya kutetea nchi na mataifa zitaendelea, kama ambavyo pia zitaendelea kupata ushindi na kufelisha njama za utawala wa Kizayuni na Saudia. Sayyid Hassan sanjari na kuashiria kuwa, Lebanon na Palestina zinakabiliwa na mashambulizi ya wavamizi, amesema kuwa uungaji mkono wa wananchi kwa harakati hizo ndio muhimili mkuu wa uwezo wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon na ni kwa ajili hiyo ndio maana maadui wanakusudia kutoa pigo dhidi ya waungaji mkono wa muqawama huo. Amesema kuwa, lengo la maadui ni kuudhoofisha muqawama na kuongeza kuwa, madamu harakati za kukabiliana na njama za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika eneo zingali zinaendelea, basi uadui pia dhidi ya muqawama pia utaendelea vivyo hivyo. Amelaani hatua ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) chini ya mashinikizo ya Saudia kuitaja Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah kuwa eti ni ya kigaidi na kuongeza kuwa, ni suala lililo wazi kwamba Saudia inatumikia tu malengo na maslahi ya Marekani na utawala haramu wa Israel katika eneo la Mashariki ya Kati. Katika fremu hiyo ametoa shukurani kwa Rais wa Tunisa Beji Caid Essebsi na Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika kwa misimamo yao ya wazi ya kuunga mkono harakati hiyo. Aidha Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya nchini Lebanon Hizbullah Sayyid Hassan Nasrullah amelaani hujuma za jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza na kusema kuwa, Ghaza imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya kila mara ya utawala wa Kizayuni na hivyo ametoa wito kwa  pande zote kulaani hujuma hizo za utawala ghasibu wa Israel.

3495365

captcha