IQNA

Iran yafadhili mashindano ya Qur'ani katika Televisheni ya Uganda

19:54 - May 28, 2016
Habari ID: 3470342
Idara ya Utamaduni ya Iran nchini Uganda imefadhili mashindano ya Qur'ani Tukufu katika Televisheni ya Kitaifa ya Uganda, UBC.
Mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Iran katika mji mkuu wa Uganda, Kampala Ali Bakhtiari katika mahojiano maalumu na IQNA, amesema, harakati za Qur'ani za idara hiyo nchini Uganda zimejikita katika masuala ya kuelimisha na kuandaa mashindano ya Qur'ani.
Ameongeza kuwa, aghalabu ya harakati za Qur'ani za idara hiyo katika kipindi cha mwaka moja uliopta ni kuunga mkono mashindano ya Qur'ani katika viwango mbali mbali vya kitaifa, vyuo vikuu, na shule.
Bakhtiari ameongeza kuwa, Idara ya Utamaduni ya Iran nchini Uganda mbali na kushiriki katika harakati a Qur'ani katika vituo vya kidini na Qur'ani kila mwaka idara hiyo huandaa mashindano ya Qur'ani katika kiwango cha kitaifa kwa ushirikiano na Televisheni ya Kitaifa ya Uganda, UBC, na mwaka huu pia mashindano hayo yanafanyika.
Ameongeza kuwa, mashindano hayo yatarushwa hewani moja kwa moja katika katika kanali mbili za UBC. Bw. Bakhtiari amesema mashindano hayo ya Qur'ani katika televisheni yatahudhuriwa pia na qarii wa kimataifa pamoja na kundi la waimbaji qasida kutoka Iran.
Aidha amesema Idara ya Utamaduni ya Iran inashirikiana na televisehni ya Kiislamu ya Salam TV katika kurusha hewani vipindi vya tafsiri na ufahamu wa Qur'ani Tukufu.
Aidha amesema idara hiyo ya utamaduni inashirikiana na taasisi mbali mbali za Kiislamu nchini Uganda huku masuala harakati za Qur'ani, umoja baina ya Waislamu, amani duniani, vijana na wanawake yakipewa kipaumbele.
3501564
captcha